
Tukio hilo lilitokea usiku wa mkesha wa Mwaka Mpya na kwamba Kazumba alifikia uamuzi huo mgumu kwa kujinyonga akitumia kamba ya katani .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alithibitisha tukio hilo alieleza kuwa “hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa na polisi kuhusu tukio hilo na uchunguzi wake unaendelea . Habari kutoka kijijini humo, zinaeleza kuwa chanzo cha Kazumba kujinyonga ni kukasirishwa na kitendo cha mkewe, Antoniata Mwisua kumnyima kitoweo cha samaki mbichi”.
Kwa upande wake mmoja wa shuhuda ambaye hakutaka jina lake liandikwe alisema kuwa “Mke wa marehemu aitwae Antoniata alimwandalia mumewe huyo chakula cha usiku, kitoweo chake kikiwa ni samaki mbichi alimkomba samaki huyo kisha akamwomba amwongezee kitoweo kingine cha samaki, lakini mkewe alimweleza kuwa kitoweo hicho kimekwisha. Ndipo mumewe alipokasirika akidai kuwa mkewe amemnyika kwa makusudi kitoweo hicho ndipo alipochukua hatua ya kuzira kula”.
Akizungumzia mkasa huo , Mwenyekiti wa Kijiji cha Kalundi , John Kalasa alidai kuwa marehemu wakati wa uhai wake alikuwa ni mtu mwenye kujawa na ghadhabu ambapo mara kadhaa alisikika akitishia kujinyonga.
Ajinyonga kisa kanyimwa kitoweo cha samaki mbichi. Duh! Imekaaje?
Reviewed by Siraj Kingi
on
16:47:00
Rating:
No comments: